Nini Tunakiona?

Maono

Miongo mitano iliyopita, kampuni hii ilijidhatiti kuwa chapa ya brashi inayoaminika zaidi nchini Tanzania pamoja na sehemu zingine za Mashariki na Kusini mwa Afrika. Katika miaka 52, kampuni imefanikiwa kufanikisha yote hayo kwa kufanya kazi kwa bidii, kuendeshwa kwa uaminifu na kujitahidi kufikia lengo. Bidhaa TBP hapo awali zilikuwa maalum katika kutengeneza brashi kutokana na mboga na nyuzu asilia na bado tunatambuliwa kama waanzilishi wa wazalishaji wa brashi za viwango vya hali ya juu. kupitia uvumbuzi na utengenezaji wa bidhaa tuliweza kufanikiwa kutengeneza brashi nyingine kadhaa kutumiaplastiki ili kutosheleza kuongezeka kwa mahitaji ya viwanda na nyumba.
Leo hii, Tanzania Brush Products inatarajia kuwa chaguo la kwanza kabisa la bidhaa za kusafisha na usafi barani Afrika na ulimwenguni kote.

director-img