Tupo Kufanya Nini?

Tunaamini Vizuri vyajiuza

Tanzania Brush Products ni chapa ya Afrika Mashariki inayotambuliwa pia Kusini mwa Afrika kwenye tasnia ya kusafisha na usafi. Mtandao wetu wa washirika wa usambazaji umekua sana katika miaka ya hivi karibuni ndani ya Tanzania na nje ya mipaka, Tanzania Brush Products sasa inatambulika kama chapa ya Kiafrika katika Nchi 9, kwa hivyo, bidhaa zetu zinaweza kuletwa kwako moja kwa moja kupitia mtandao wetu wa kimataifa. Tunachojitahidi ni kutengeneza bidhaa ambayo inazungumza ubora na wakati huo huo inaweza kuwa bidhaa ambayo watumiaji wa aina tofauti wanaweza kumudu.

director-img

Vitu vitatu vinavyofafanua sisi ni nani na kwanini sisi ndio chaguo la kwanza la wateja:

  1. Tunaamini sana katika kusikikiza maoni ya wateja wetu.

  2. Tumejenga msingi bora kabisa wa mawasiliano baina yetu, wateja wetu, watumiaji wa bidhaa au wafanyikazi

  3. Tuna bei shindani na bidhaa zenye kudumu muda mrefu.

Tunaendelea kujitahidi kuiweka Tanzania kwenye ramani, kama moja ya viongozi kwenye swala la utengenezaji na viwanda barani Afrika, haswa katika uwanja wa bidhaa za kusafisha na usafi.